E-Sir
Lyrical Tongue Twista
[Intro]
Baba, mama, kaka, dada
Auntie, uncle
Mamanzi, mabeshte, wanati
Ma-producer

[Verse 1]
Kila mtu anashuku vile mtiririko huu wa huyu ndugu
Umeingia Nairobi na kusambaa kwa miji kama Nakuru
Na kudhuru ubongo, si uwongo
Kupendwa na kila mtu kama label ya FUBU, nafikiri
Labda ni vile nabwaga zawafanya mnataka kunihanda
Kuniweka nyuma ya Canter, kunivukisha mpaka Tanzania
Na isipowezekana Somalia ama Uganda
Lakini hai-tawezekana vile nabamba ni kama stima na maji ikishikana, danger
Kila wakati natema wanapenda, wanasema tuangushie tena
It's the number one rap contender
Niliona mahali pa kupita nikapenya
Sasa December to December, nitaendelea kuwaletea chapter
Baada ya chapter ya huyu kijana anayepepea
E-sizzle

[Hook]
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
(E-sizzle, matatizo)
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
(E-sizzle)

[Verse 2]
Kwa hivyo flow ukiitaka
Pole pole ikifuatiwa na haraka au vice versa, kaka au dada
Uliza na sitasita kukuangushia flow inayofanya kichwa kwenda mbele na nyuma ikionyesha mishipa
Na Mister E dash, pewa cash
Mnati, pewa mbili kwa kitambi
Nachukia wanaonichukia vile nachukia kufanya dhambi, basi
Nawa-ignore na kufanya vile nafanya kwa amani
Better yet, kama wimbo wa Shaggy, nice and lovely
Ukijia pesa zangu, naleta ukali
Zamani nilikuwa si-mix business na pleasure
Well, guess what? Bado sizichanganyi, samahani
Nimesahau kukuambia hisia kukusaidia ku-party
E-Sir ya-rock flows, utafikiri Nas na Jay-Z wamekuja Kenya
Ama Tupac na Biggie wame-resurrect tena
(E-sizzle)

[Hook]
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
(E-sizzle, matatizo)
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
(E-sizzle, matatizo)
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?
(E-sizzle, matatizo)
Ni E-Sir! (E-Sir!)
Pewa mbili kwenye kichwa
Lyrical tongue twister na Mister K-I-swahili
Nani yuko na shida na mimi?