Lava Lava
Tuachane
[Intro]
Aaaaah Aaaah Aaaaah Aaaah

[Verse 1]
Kama Imeshindikana Kunirudia Isiwe Taabu
 Usiuforce Moyo Kupenda Usipostahili
 Ya Nini Kung’ang’ania Nishachoka Kuwekwa Sub
 Siwezi Ooh Na Mapenzi Nishaghaili
 Tena Niko Tayari Vipigwe Vinumbi Kengere Kwa Sherehe
 Kinaghaubagha Mbele Ya Umati Tuachane
 Na Kama Hautojali Tuite Waumini Mapadre Na Masheikh
Yaishe Labda Sa Kwa Nini Tutesane 
Kweli We Ndo Nikupendae Ila Unanipa Ghadabu Jina
 Tusitoane Nyongo 
Na Kama Umenichoka Eh Niache Kistarabu Jina
 Usinipe Chongo Miee

[Bridge]
Mwili Umebaki Kongoro Nyama Sina Ni Mifupa
 Naiona Ndomboro Kabisa Siwezi Furukuta
 Penzi Kiporo Limeshachina Linanuka
 Huishi Kokoro Purukushani Kutwa Kucha Iyeeh

[Chorus]
Bora Tuachane Bora Tuachane Siwezi
 Bora Tuachane Yamenishinda Mapenzi
 Mi Naona Bora Tuachane eeh Tuachane Siwezi
 Bora Tuachane Yamenishinda Mapenzi

[Verse 2]
Ni Dhahiri Kisima Kimekauka Maji
 Ndo Maana Naona Kata Sina Maana Tena 
Nilifikiri Mi Gonjwa Langu Limepata Mponyaji
Umeniongezea Homa Mwili Wote Wantetema
 Mi Naona Basi Labda Si Ridhiki Yangu
 Kama Hunitaki Acha Tu Niende Zangu
Ya Nini Mishikaki Ntatafuta Boda Yangu
 Nijinafasi Niipande Peke Yangu

[Bridge]
Mwili Umebaki Kongoro Nyama Sina Ni Mifupa 
Naiona Ndomboro Kabisa Siwezi Furukuta 
Penzi Kiporo Limeshachina Linanuka
 Huishi Kokoro Purukushani Kutwa Kucha Iyeeh

[Chorus]
Bora Tuachane Bora Tuachane Siwezi Bora Tuachane Yamenishinda Mapenzi
 Mi Naona Bora Tuachane Eeh Tuachane Siwezi
Bora Tuachane Yamenishinda Mapenzi