Harmonize
Nani
[Paroles de "Nani"]

Mmmh yeah
Mmmh
Yeah, (Moko)

Asubuhi kumekucha
Wingu limetanda
Na mvua yata kunyesha
Na uko mbali Mama

Maji takitirika
Ooh baridi itanishika
We ndo chanda chema
Uhakika unanitatisha tamaa

Utaambiwa binadamu
Ah kila mmoja ana mapungufu yake
Sijui nilipoteleza Mama

Si ungenambia
Nime miss tabasamu
Kutwa kucha
Picha kumezea mate
Yangu fimbo umeibezea
Ah katu hautaki kuitumia
Labda hesabu za kutoa
Mi niligawanya baby unisamehe
Na ile hasi nikaifanya chanya
Baby unisamehe

Na hata emoji za kulia
Nazo kutumia nazo zikome
Japo nipate furaha
Ah huruma unionee

Maana hii hali, hata haifichiki
Kutwa wima kwa mpingo, kisiki
Maana hata nikiona michezo ya njiwa
Ah hua naitamani

Kama si wewe

Nitampenda nani?
Nitampenda nani?
Nitampenda nani
Nani nitampenda

Nitampenda nani?
Nitampenda nani?
Nitampenda nani
Nani nitampenda, aah
(Uuh)
Eeh penzi usifanye kwa chombo cha usafiri
Ikawa umeshuka ujе utanikatili
Nitakuwaga mental, niko dhahari
Si unasikia

Penzi la dhati daima la wawili
We fanya urudi lisiwе batili
Ka wafanya kusudi ni ukatili
Mi naumia

We ndo yangu hifadhi
Labda nilikosea msimbo
Kweli kupenda kazi
Wangu umegeuka fimbo o

Mi ndo lako koroboi
Lile lisilozima
Aah si ulisemaga hauchomoi
Kumbe imani unanipima aah

Pia ulisema haudonoi
Wameiteka mazima
Ahaa simun'gunyi, sikohoi
Sina vyangu nimechina
Maana hii hali hata haifichiki
Kutwa wima cha mpingo, kisiki
Maana hata nikiona michezo ya njiwa
Ah hua naitamani

Kama si wewe

Nitampenda nani?
Nitampenda nani?
Nitampenda nani
Nani nitampenda

Nitampenda nani?
Nitampenda nani?
Nitampenda nani
Nani nitampenda, aah