Mbosso
Shida
[Verse 1]
Natoka zangu kwetu Kibiti
Naisaka Dar es Salaam
Naenda tafuta riziki
Niwatunze Baba na Mama
Nikizunga haba na haba
Ndio kilo inatosha
Chunga miguu kuvaa Rubber bana
Zisizo kutosha
Anayesema riziki mafungu saba
Anakupotosha
Riziki mafungu mawili
Kupata au kukosa
Aliyoyasema baba
Heshima ya nyumba si dirisha
Dunia ni saa mbovu mwana
Usije ifwatisha
Vingine vinakaba
Lazima unywe maji kupitisha
Umia upate kovu baba
Maumivu yatakwisha

[Bridge]
Hata mate kinywani ya uchungu
Nayameza kwa tabu jama
Maisha yangu mazingaombwe
Ya maajabu sana
Oooh mama Oooh
Eeeeh mama eeeh
[Chorus]
Ooooh Shida Ooooh Shida
Ooooh Shida Ooooh Shida
Shida zitakwisha lini
Ooooh Shida Ooooh Shida
Ooooh Shida Ooooh Shida
Shida zitakwisha lini

[Verse 2]
Najipa matumaini
Nitafute nisichoke
Moyoni nikiamini kuwa
Mungu ni wetu sote
Ila Mbona kwangu sasambu sasambu
Sipati usiku si mchana
Ama kitabu cha riziki yangu
Tayari kimechanwa
Eeeeh eh Eeeeh
Baba Mama chama na mogela
Yani mimi ndio nategemewa
Nakaza nashinda kombolela
Likipigwa nabutua hewa

[Bridge]
Hata mate kinywani ya uchungu
Nayameza kwa tabu jama
Maisha yangu mazingaombwe
Ya maajabu sana
Oooh mama Oooh (Oooh)
Eeeeh mama eeeh (Oh Oooh)
[Chorus]
Ooooh Shida (Ooooh Shida)
Ooooh Shida (Ooooh)
Ooooh Shida
Shida zitakwisha lini (Mama mama eeh)
Ooooh Shida (Mama mama eeh)
Ooooh Shida (Mama mama aaah)
Ooooh Shida (Ooooh)
Shida zitakwisha lini