Intro:
Mwenyewe anaona sawa
Ila mwambie mimi ananiumiza sana
Ni zaidi ya kupagawa
Siponi ugonjwa na nishamaliza dawa
Verse1:
Na ajue bado nipo
Ila hali yangu hohehahe
Sina mabadiliko
Machozi mafuriko fundi wa jiko langu kaacha mawe
Mpaka akalamba mwiko
Bridge:
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi
Chorus:
Mwili watepeteka
Sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari
Naanza dhoofika
Mwili watepeteka
Sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari
Naanza dhoofika
Verse2:
Bado ndo ndo ndo chururu
Nikijaza haikai kibaba
Na misongosongo msururu
Sita haikai saba
Mimi kitorondo ye kunguru
Mbao zangu hazimpi msaada
Makombe nishaoga dawa ka susuru
Huenda nikasahu labda
Kitandani mito ipo miwili
Ubavu wewe ubavu mimi
Pakata ndiko imewekwa shubiri
Nalikwepa nalala chini
Nimefuta picha tulizopiga chumbani
Ila bado zanisuta suta zimebaki kichwani
Silali nastuka stuka unaniita gizani
Chozi lalowesha shuka na sina wa kunifuta nani
Bridge:
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi
Chorus:
Mwili watepeteka
Sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari
Naanza dhoofika
Mwili watepeteka
Sina afadhali mawazo yanitesa
Mbavu dabodeka ni ka misumari
Naanza dhoofika
Outro:
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi
Toka alivyoniacha
Sina nyota wala mwezi
Mwenzake nimekamatwa
Na homa ya mapenzi