Mbosso
Nipo Nae
(Ayolizer)
Masikini hana fuba, hana fuba
Anazeeka yule mwezangu
Haamini anavyochunda anachunda
Nimeondoka na nyota yangu

Nafsi ilichoka madhira (Ooh madhira)
Ya pundazo na fadhila (Ooh fadhila)
Nimempata wa njema dhamira (Ooh dhamira)
Wa kufunga magoli si wa bila (Ooh wa bila)

Mmmh shata shata (Shata)
Penzi limetaradadi
Sina shaka (Shaka)
Inyeshe na ipige radi

Rasha rasha (Rasha)
Kwetu mambo maji maji
Baby washa washa (Washa)
Waambie wanaosubiria

Bado nipo nipo nae
Bado tupo sana tu (Bado nipo nipo nae)
Ndo kuanza tunayaanza (Bado nipo nipo nae)
Wenyewe tumeshazoeana (Bado nipo nipo nae)
Mi bado nipo na yeye
Msitufuate, msitufuate
Msitufuate, msitufuate

Raha, raha mstarehe
Sijaomba napewa
Nifikishwe nitosheke
Raha kila siku sherehe
Jamani nanyenyekewe
Eti nile nikogеshwe

Penzi birika, yake sifai ni kimiminio
Ah nimеshikwa, kwenye kichwa mpaka masikio
Mambo tartita, ulichosusa hakula mwenzio
Mwana ana sifa, ananipa paja kwa kipapatio

Amekupenda mama tulia tulia
Tule zetu ni ujana, dunia dunia
Mambo ya wanadama, puuzia puuzia
Wapasuke bandama, sindano ishawaingia

Mmmh shata shata (Shata)
Penzi limetaradadi
Sina shaka (Shaka)
Inyeshe na ipige radi

Rasha rasha (Rasha)
Kwetu mambo maji maji
Baby washa washa (Washa)
Waambie wanaosubiria
Bado nipo nipo nae
Bado tupo sana tu (Bado nipo nipo nae)
Ndo kuanza tunayaanza (Bado nipo nipo nae)
Wenyewe tumeshazoeana (Bado nipo nipo nae)
Mi bado nipo na yeye

(Wasafi)