Mbosso
Haijakaa Sawa
Sasa unanuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mlenda

Siko juu siko chini
Niko nusu sadoo
Sio wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado

Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane
Tena nafunga na Suna
Mambo bado bado mwana wane
Naona yanazidi kuguma

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Haijakaa sawa
Nivumiliye ipo siku tutapata
Haijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Haijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Haijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama
Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuming'inya
Pokea kidogo changu
Tunywe chai na mkate wa kumimina
Akili ikichoka riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza
Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu
Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivu
Na kwenye waliopo tumo
Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyee eeh eeh

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Haijakaa sawa
Nivumiliye ipo siku tutapata
Haijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Haijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Haijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama