Intro (Ghafla)
Yaaah
Aah aah
Love
(Dobe Pro is on a track)
Verse 1 (Ghafla)
Je utanifaa?
Nilichopata ndo nilichoweza,Je utakula?
Najua kuvaa
Unajua kung'aa,Je utaweza maisha ya kuunga?
Najua ujamaa umeshakufa
Inabidi nijitume peke yangu pesa ya sabuni usije nuka
Niweke msosi mezani usije konda nguo zikavuka
Umenihifadhi zaidi ya usichana kwenye mwili wako najua ni mimi
Umeniweka kwenye moyo wako sasa kidole pete ya nini
Shugamami wapakata vijana kwenye mapaja kisa mkwanja hawanipati naomba uniamini
Sasa nimekuwa sipo na mama nahitaji njia,nia ipo
Mwanamke wa kuishi nae mpaka nafukiwa,achana na hawa vicheche miyeyusho
Najua unajua maana ya dhati,Ni hatuachani mpaka maandiko yatimie
Kwamba huu ndo mwisho wa uhai wewe au mie
Na utanikumbuka ndani ya udongo,utatamani hata fuvu
Utatamani tuzikwe wotе,damu moja zaidi ya undugu
Ni sisi (ts goo)
Chorus (Jay Melody)
Ni mahali gani unatamani naweza kukuonyesha (aah) au unadhani sio muda huu
Nyumba magari na ufahari nikipata pеsa,unaona maisha yalianza kwa mguu
Shoga zako na mashosti watakupoteza (aah)hiyo inanipa mashaka
Sema
(Mashaka unanipa mashaka mashaka)X3
Easy
Verse 2 (Ghafla)
Na ukinikosa usiku mmoja utaumia sana usilaumu roho
Unahisi nipo bar nakunywa nafuja unapiga simu Ghafla njoo
Muda mwingi nipo studio au chimbo uandishi
Nimesoma kuondoa lawama ila chakula changu ni mziki sikufichi
Siku ukileta changamoto hautonikimbia niahidi
Maisha ya kununua navaa
Navua nafua inang'aa na kisha naivaa tena
Fataki akikuita kataa
Akikupa chapaa,Je unaweza ukalegeza?
Vijana wanauza hisia zao kwa shetani kisa pesa
Nayakabidhi maisha yangu kwa Mungu baba yeye ndo muweza
Kwenye usaliti kuna njaa
Bado nina hofu na huu wasaa
Moyo mchovu nimechoshwa na mapenzi jamaa
Na shost zako wakikuambia nina hit and run kataa
Sikuchezei tutachezea pesa(hahaha) furaha
Na nitatafuta mpaka waniite jina, shujaa
Napata hofu siku ukiondoka hivi nitadondoka nitakaa?
Nitashindwa kusimama kisa mrembo umenikataa?
Ndio nitaumia ila sirudi nyuma mi ni sehemu ya mitaa
Chorus (Jay Melody)
Ni mahali gani unatamani naweza kukuonyesha (aah) au unadhani sio muda huu
Nyumba magari na ufahari nikipata pesa,unaona maisha yalianza kwa mguu
Shoga zako na mashosti watakupoteza (aah) hiyo inanipa mashaka
Sema
(Mashaka unanipa mashaka mashaka)X3
Outro (Jay Melody)
Ni mahali gani unatamani naweza kukuonyesha
Nyumba magari na ufahari nikipata pesa
Maisha yalianza kwa mguu
Mashoga zako,mashosti..
KSS STUDIO