King Kaka
East Kwa Mabeast
Ok
King Kaka
Karibu East Kwa Mabeast
Nyanyangu aliniombea niwe na macho kwa kisogo incase nagwaya
Si dwell in the past but hiyo past imeni insipre
Na vile kuna noma sahii wajanja ka mimi watajenga bridge, wajinga ka Patel watajenga dam
Ka hauwezi beba maarifa usijichoche unaweza cram
Si unikose basi ndio nijue nia, si tupotee basi ndio tujue njia
Si kuna sewer zimepita kwa living Eastlando na hauwezi throw up
My prayer tu ilikuwa niweze grow up
Closing day nimengoja hadi three na dad hakushow up
Sijakushow kwetu tulikuwa best friends na njaa
Ceiling yetu haikuwa best friends na taa
Nyi mko na timetable kwa fridge vile ile food mtadecide
Tulikosa sana I think minyoo zangu zili commit suicide
Eyewitness ya death ya akina Ronnie na Ndishu
Kwanini mother aliharibu, schoolfees na maisha inaweza teach you
Sijawai get comfortable, hii sio kitambi nimestomach issues
All along wametushow sisi ni others, sisi ni ETC
Hesabu haziingi, kumbe ni syllabus ya IEBC
Hawakutunyunyuzia maji basi hatuwezi koma
Na wewe hautaki ku obey basi hauwezi command
Tulitamani sana hiyo life ya top za Hawaii, jinika tight na masahara
Doh beside them, chuma kwa buckle na madem na mascara
Hadi ile siku OCS alikutana na wao akawaambia basi lala
Si we ndio umekuwa ukihangaisha hii mtaa usiku na mchana
Ile panya inauma ikipuliza si imepatikana
Next week tulikuwa tunaenda ocha kwao na basi saba
Nikachujwa chuo mara kadhaa na ata nikawish niende
East kwa workshop ya devil nikawish Fe nibebe
Thank God kila weekend niko kwa class, I mean first class kwa ndege
Na akili zikiwa uji si wataenda kwa chief kukesi
We una chase madem, si uchase doh na madem watakuchesi
Si uhave dialogues na God, hawajakushow vile ameniblessings
Umeblessiwa kwa dias ya cathedral
Jiulize mbona pastor haendi kuperform miracles kwa hospitals
Sikuhizi ata church iko na madingo na gospel iko na Willy Paul
But I don’t judge, mi nangoja siku maJudge watajudgiwa na God
Shule ya rap niligraduate from sunguch to a GOAT
Umeshindana na elephant kushonde, hapo ndio itawacost
Private wing daktari atakuwa anatie kaKnot
Birthday zilikuwa githeri na mabaloons
Sahii ni private rooms na round table ni ma tycoons
Ntanawa bado ata kuku ikiletwa even though kuna a knife na five spoons
Na huyu politicians ni mjinga aje?
Ndani ya SUV anajificha aje?
Actually si ndio wajinga aje?
Na kura bado tutapiga aje
Potholes zinahitaji lifeguard juu zimejaa maji
Na akipita ako na five cars, ohh reminder hiyo ni ganji yako yaani your tax
Basi parliament iitwe bedroom
Huyu tu ni Kaka anawa attack, hizo manifesto ni whack
For the last time mi sina beef na Sauti
Mi niko na mabiz huko Saudi
Wanilock niko kwa bars ka kauzi
Na vile mzizi iko deep ntaogopaje upepo?
Bado KING ata mkitamka potato potato
Naangalia kwa kioo na everything I need inaniangalia
I smell fear vile tu kwa kila room naingia
I mean rappers, rappers, rappers
Mnataka kumaliza career zenu basi dai verse
Unataka kupendwa na kila mtu basi die first
Tunalive the dream utakuwa aje na nightmares
Dr. King alishafight for the Dream ndio tusikuwe na nightmares
Ndio maana kila night na make love na success kwa bed
Remember, patience puts a crown on the head
Karibu tu feast
Karibu EAST KWA MABEAST