Rahul
Mtoto wakiafrica
Chorus:
Mtoto wakiafrica nakupenda- jinsi Olivyo umbika ni wewe tiu
Macho yako wewe- unavyo ya rembua Mimi kwako kweli ni meditate
Verse 1
Ni wewe nikupendaye- wangu ulo na thamani
Na ndiwe unifaaye- mjuzi kwenye makini
Katu sikuachi miye- wakerekao poleni
Chorus
Verse 2
Mimi nakutaja wewe- wangu baby mahashumu
Simuoni mwenginewe- na hili piya fahamu
Hata sumu tuekewe- mi nawe hadi kiyamu
Chorus
Verse 3
Basi imani fanyiza- unitowe kwenye taabu
Usiwe unaniliza- mpenzi wangu swahibu
Ukini fanyia iza - mwenzio wani adhibu
Chorus
Verse 4
Moyo wangu umependa - uwe wangu laazizi
Usini fanyie inda -jicho likatowa chozi
Hebu sema wanipenda - niridhike nalo Penzi
Chorus
End