Diamond Platnumz
Bado
[Intro: Harmonize]
Wasafi
Instrumentals
Wasafi Records
Ah, ah
Mmm

[Verse 1: Harmonize]
Kutwa kidomo wazi, nikifuta na machozi
Huku namuomba Mola unitoke moyoni
Ila ndio siwezi, nakesha ka mlinzi
Maana hata nkilala unaniijia ndotoni
(Lato)
Asante kwa kuniumiza
Nimejifunza mengi, mwanzo sikuyajua
(Katu)
Naapa kutolipiza
Ila mwambie mapenzi abaki kuyasikia, eeh, eeh
Nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia, utabaki nami
Tena ukala na viapo, 'Taurat, Bibilia
Leo sikuoni

[Chorus: Harmonize]
Ila mwenzako bado
(Bado, bado, bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado, sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado, bado, bado bado)
Mmm, bado
(Bado, bado, sijapona)
Misijapona roho
[Verse 2: Diamond Platnumz]
Mmm, mm
Aa-ah
Mola, nishike mkono baba muumba
Haya ninayo yaona, simanzi
Ah, yaani bora 'jicho mchanga ningefumba
Huenda ningeshapona, maradhi
Oh, maumivu yangu, hayawezi kupona kwa vidonge
Sababu panapo nichoma, nikipapasa sipaoni
Kweli pekee yangu, umeniacha na unyonge
Kabisa wakanipokonya tonge langu mdomoni

[Pre-Chorus: Diamond Platnumz]
Onana, nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia, utabaki nami, ih
Oh
Mi ndio mwili, mi roho yako
Yaani umetimia, mbona sikuoni
Ila mwenzako mimi

[Chorus: Harmonize & Diamond Platnumz]
(Bado, bado)
Mmm, mm
(Bado, bado)
Mwambie bado
(Bado, bado, sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado, bado, bado, bado)
Mmm, bado
(Bado, bado, sijapona)
[Bridge : Diamond Platnumz]
Ah-ah'
Ile roho yangu mama
(Ibebe)
Inanidondoka
(Ibebe)
Iokote mama
Ibebe, chaukucha nsije zima
Ooh, roho yangu
(Ibebe)
Inanidondoka
(Ibebe)
Njoo unishike mama, ooh
(Ibebe, chaukucha nsije zima)
Ah-ah, ai wewe
(Ibebe)
Watanizika mama
(Ibebe)
Mwenzio taabani
(Ibebe, chaukucha nsije zima)

[Bridge : Harmonize]
Mmh
Masikini pendo langu
(Ibebe)
Linandondoka
(Ibebe)
Niokote mama
(Ibebe, chaukucha nsije zima)
(Instrumentals)

[Outro: Diamond Platnumz]
Ibebe
Ibebe
Ibebe
Chaukucha nsije zima
Ibebe
Ibebe
Ibebe
Chaukucha nsije zima