Diamond Platnumz
Ntaanzaje
(Ayolizer)
Aliumba ardhi akaumba mbingu
Akaumba mbaramwezi
Kaumba nafsi, kaumba wivu
Akayaumba na mapenzi

Na kukuacha sidhani, siwezi jaribu
Maana penzi kwa mzani, umenizidi mahabibu
Shika vyema usukani, twende taratibu
Baada ya tuta baby koleza gear

Yaani tam tam kama pipi
Nakuita sweet, ah lote lote
Fundi kwenye kwichikwichi
Shape vipi? Kama lote

Vicheche nisha delete
Sitaki cheat, wa toke toke
Kwenye moyo nimekupa seat
We ndo dereva, so kukuacha oh

Naanzaje? (Ooh mimi)
Naanzaje? (Aah mimi hapa)
Naanzaje? Mwenzako kukuacha siwezi

Naanzaje? (Ooh mimi)
Naanzaje? (Aah mi jamani)
Kukuacha oh, kabisa siwezi
Hadithi kuja hadithi njoo, utamu kolea
Mwezenu huba liko kwa roho, limeninogea
Vishenshuda poleni woo, mnalo wambeya
Mtaja kuumwa makwashakoo, kwa kutuongelea

Tena me kwake ndo daktari, nampa tiba halali
Wanaitaga sukari, alamba haa!
Na jana nilifunga nikasali, nikamuomba Jalali
Tuepushe madhohari, ya wanadamu

Ah ah, we mtam tam kama pipi
Nakuita sweet, ah lote lote
Fundi kwenye kwichikwichi
Shape vipi? Kama lote

Vicheche nisha delete
Sitaki cheat, wa toke toke
Kwenye moyo nimekupa seat
We ndo dereva, so kukuacha woo woo

Naanzaje? (Ooh mimi)
Naanzaje? (Aah mimi hapa)
Naanzaje? Mwenzako kukuacha siwezi

Naanzaje? (Ooh mimi)
Naanzaje? (Aah mi jamani)
Kukuacha oh, kabisa siwezi
Na kukuacha sidhani
Siwezi jaribu
Maana penzi kwa mzani
Umenizidi mahabibu

(Wasafi)