Fid Q
Tajiri Yangu
-Chorus(Paul Clement)
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yangu

Verse 1(Fid Q)
Lord, ni ngumu kujua we uko wapi ila unajua nilipo
.Naiska haki kuipata ni bahati
Vyuma vikiza najichangachanga kuusaka mshiko
Na mbanga zinakwaza madada wa kudanga wanabamba vifo
Na waliopinda we uwalinde nolove
Ka wale wajinga walionipinga napowinda wokovu
Haunipi shida bila namna kuisolve
We ndio mmiliki wa kila tiba na hauna roho mbovu
Hauna roho mbovu unanipa incharge na power ninyanyue juu
Ni zaidi ya dawa sikuhitaji ninapougua tu
Unaniweka sawa devil akitua hamchukui Q
Una uwezo wa kunigawa au kuniumbua sio tu kuniumba mkuu
Ni rhumba tu ndio linaweka vumba juu na kututesa kama mfungwa aliyechoka kudundwa juu
We ndio BOSS ninaekuamini haututosi tukichomewa
Sio wale wanaowahi kazini ili wafoke tukichelewa

[Chorus](Paul Clement)
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yanguVerse 2 (Fid Q)
Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza
Anakwapua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza
Hii inafanya nafsi yangu ikose subira
Ikose usingizi, uoga huzuni niwe na hasira
Kwangu furaha nikiwa na MUNGU sio mlungula
Na pia siku zote mla raha na chungu hula
Najua nilipotoka, najua wapi nilipo isipokuwa ni we pekee unajua lini nitafika mwisho
Cheo chako ni kirefu zaidi ya dunia
Kipana zaidi ya bahari, ulinzi mkali hakuna askari anaefikia
Namlaani shetani kiundani nipate kujua mkuu
Ili nijihami na mtihani nisiache tusua Q
Najua una huruma naomba nikibuma usinitose
Mwanadamu atazingua heshima sio utumwa kwa Boss
Hauwezi nunua uhai sasa najidai kwa lipi?


[Chorus](Paul Clement)
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
Ewe, Ewe tajiri yangu
Wewe ndiwe kila kitu kwangu
We ni tajiri, wa matajiri
We ni tajiri, tajiri yangu

[Bridge]

Siwezi kuwa masikini sababu
Anaenitunza ni tajiri ni MUNGU
Asieacha nigange njaa, nikose furaha, nikate tama
Ewe Ewe tajiri, yangu
We ni kila kitu kwangu
Umebeba uhai wangu
Umebeba maisha yangu
Tajiri wa uhai wangu
Tajiri wa maisha yangu
Tajiri wa kila kitu kwangu