Fid Q
Hustle
[Hook: A.V.I.D]
Mmmh!
You know I hustle/
I hustle/
Haaard..
I hustle/
I hustle/
Haaaard..

[Verse 1: Fid Q]
Naongeza maujuzi ili nisichokwe na crown, Heeenh/
Usilete makuzi, Hamtaki nitoke na bounce, Heeenh/
Ni mzee mbuzi, SHIPAPI, Zitoke hizo blouse, Heeenh/
Take off the shoes when you walk in the house/
Na hurudi ndani kama futi ya fundi ukuta/
Nina bahati f'lani mamluki, Wazushi hunisusa/
Kesho sio spesho, ikiwa haifiki ka keshokutwa/
Na ni vyema depo usiwepo, ikiwa street we ni kuruta/
Na je mnaamini kwenye Get up and get it/
Au ndio mshalemazwa na ile sit down and see it/
Siri ikiwa ya wawili haiwi siri mtaji Snitch/
Na tajiri haukariri, Hauoni watabiri wana-switch/
Mko bize, Mnataka mniharibie nisitoke/
Njia yenu ina utelezi, Nije mnipatie matope??/
Mna upungufu wa umakini/
Mnahitaji rapture kama waefeso/
Luni ki nne kumi na saba/
Sometimes, Nakaa chini akilini najenga fikra/
Najiuliza lini mtashika madini ya hichi kichwa/
Ukauzu huu sio wa kufuga kama mzuzu wa Zavara/
Msi confuse Kung Fu na ile Lugha ya ishara/
Na flip hii game, kama Jaguar kwenye maonyesho ya sarakasi/
Kwa mademu mi zaidi ya viagra inayompa msaada bwana yake/
So.. Nikimwona mchizi, Anam kiss demu wangu wa zamani/
Kwenye Lips na ana enjoy nahisi atamu yule demu akinipa m... Sikojoi/
[Hook: A.V.I.D]
I hustle/
Haaard..
I hustle/
I hustle/
Haaaard..

[Verse 2: Fid Q]
I want some mother shit ka dudu kuwa kwenye tundu sio, Huuh??
Unaweza ukauwa ukawa na uchungu na kilio, Huuh??
Nachojua kiwe sure kiwe ndiyo, Huuh?
Tusiwe waoga unataka slogan?? ndiyo hio, Huuh?
Naona mnavyonifonza napoonja mafanikio/
Jeshi la mtu mmoja sitochoka, Sitotoka mbio/
Sitotoka na kiu ya mgonjwa aliyeponzwa na kauli mbiu hiyo/
Nakufa moyo nikikwama imani inakosa/
Kichwani zinatoka, Nani wa kumlaani haswa unanitosa/
Kwa sehemu husika ni vyema, Game linalipa mapema/
Ukizishika neema, Hunipa kwa fani ya kufoka/
Kisha unasema mlaji sio mchumi, Huunh??
Namvisha taji uvunaji unahitaji kanuni, Huunh??
Inakuwaje sina kumi wakati nina tisa/
Watanijuaje muhuni bila kusababisha/
Kama mapacha na DO ME, Au May Weather na ngumi??/
Juu ya meza au uvunguni, Bila kuwekeza hata thumni??/
Nachokieneza hakibumi, Haswa wakinipigisha bars wao huteleza/
Sio wakati wa R. Kelly wamwache Chris Breezy atishe/
Akiwa Lubumbashi au na hii chart na Ekotite, Eeeh?/
Anataka apite, Abaki kati ili bahati isimshike/
Asitambae na chaki mvute shati hisabati zimtishe/
Dharau ndio kilema nilichonacho/
Nawasahau mapema wadau walionitema kisha na hustle/
Na ninapiga bao, Vyema mbele yao/
Tena wakiwa macho, Nyamazisha wanao/
Nena kwa Neema nikivuja Jasho/
Mziki ni zaidi ya DO RE MI FA SOOO/
Na wapenda kiki ndio wanalowea mipashoo/
Na ninasikia siku hizi pesa inafanya upuuzi uwe ishu/
Kisa inalipa isiwe excuse kwa kila kitu/
[Hook: A.V.I.D]
I put my heart and soul, coz this all i know/
All I know is to hustle/
I hustle/
I hustle hard/
You know I hustle/
You know I hustle/
Haaard/

Wanene