Fid Q
Ni Hayo Tu
Intro:
Oyaa, dogo, we mshamba we njoo hapa
We ndio wanakuita Fid Q, (Ndio)
Hebu atupe mistari kwanza...

[Verse I: Fid Q]
Korombwea hayo maisha ya kuungaunga, hiyo shughuli mi naiweza
Hapa utaambulia ushauri ukihitaji msaada wa kifedha
Mi kujiita rasta, wenye chuki tu wanapinga
Wanashangaa na kula nyama, hawajui nyota yangu ni ya simba
Asiye fikiri kabla ya tendo, atatendwa pale akidamka
Na usinidiss kwa kiswahili kama hujui hata kukitamka
Kuongea sio kusema na kufumbua macho sio kuamka
Wasiwasi ukiwanyima raha, mistari itawafanya kuchangamka
Mnapagawa na baadhi ya mambo ambayo nayajua
Pia nna uwezo kufanya mpaka madawa yanaugua
Hii ni I level, sio high level ndio maana hunioni
Waulize wenzako, Fid Q yupo juu zaidi yako homie
Nipo juu, je utanibana kama kizibo cha soda?
Kushuka ngazi tu unahema, je kuzipanda hupati uoga?
Amini usiamini, Fid Q ndiyo sauti ya mtaani
Je, mtafurahi nikishuka chini kama mademu wa marubani
Bora kuogopwa, wakikupenda watakuchukia
Nilipo na nilipo anzia, sipo napo hitaji nibaki pia
Si hofii kupitwa ilimradi muda usiniache
Hii ni kwa wote, popote
Siogopi kuomba mvua najua mnayahofia matope
Mwingine anakurupuka ananiiga, anasema sifai
Naona vibaya kumjibu, sahau kutupa mawe juu ya mayai
Chipukizi chapeni kazi ili mng'atuke mlipokwama
Vumilieni kama nyota mtatoka jua likizama
Ni binadamu sijakamilika, kuandika rhymes sikosei
Japo miluzi ni mingi lakini jibu huwa sipotei
Nitaendelea kuwa mshindi wa juu ka majani na record Bongo
Nakutembea kifua mbele utadhani nimedundwa ngumi ya mgongo
(Aargh, Fid Q kitu gani bwana...)
(Afu mi ananikeraga anajifanya anapenda mademu wa kizungu)
(Achana nae, nyie asikuzingueni Bongo fleva kitu gani...)
[Hook: Fid Q]
Kila mtu Fid Q hivi, mara Fid Q vile
Yaani Fid Q, Fid Q, Fid Q tuuu, ni hayo tu
Kila mtu Fid Q hivi, mara Fid Q vile
Yaani Fid Q, Fid Q, Fid Q tuuu, ni hayo tu

[Verse II: Profesa Jay]
Ukinicheka shambani, mi nakucheka sokoni
Chuma au fua chuma, ni mwendo wa roho mkononi
Maisha ni mpangilio, ukitulia yanajiseti
Ni kama A to Z kwenye mfumo wa alfabeti
Hawara hana takala, ukimtaka unampata
Bendera ibaki hewani, natimba chaka kwa chaka
Hatufanani kama alama za vidole
Na bado naziamini falsafa za mwenda pole
Unaishi nyumba ya vioo, basi usinitupie mawe
Heshima yangu sikuipata katika sandakalawe
Inakuwaje unadiss? unampaka wa mawazo
Unazungumzia ujazo, milazo au micharazo
Nilichuna wakati wa kwenda, ila sasa narudi
Nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi
Ni hayo tu, kama hujitumi piga mihayo tu
Fid Q na Jizze heshima ndiyo tuitakayo tu

[Hook: Profesa Jay]
Kila mtu profesa hivi, mara Profesa vile
Yaani Jay profesa? Jay tuu, ni hayo tu
Kila mtu profesa hivi, mara Profesa vile
Yaani Jay profesa? Jay tuu, ni hayo tu
(..jana nilimuona maskani, kaja na kipensi rafiki yangu
Afu sijui kanywa gongo alafu ile Benzi lao analisukuma halina mafuta..)
(We mwenyewe unamuonaje kwanza?)
(..njaa.. anapenda tatizo mimamaa..)

[Verse III: Langa]
Natumia akili, ustaarabu, na subira
Situmii mwili, jazba, na hasira
Mapinduzi daima, msimamo ka Che Guevara
Usingizi ndugu yake kifo, sipendi kulala
Nafuata mipango yangu, sifuati mipango ya wengine
Niko focused, hata ikibidi vingine nijinyime
Wote tukiwa masikini, nani atamsaidia mwenzake?
Niacheni ni win, majungu msinipake
Wanasema nimechange, eti sio mimi wa zamani
Sionekani maskani kwa darubini wala miwani
Lawama kibao utadhani mahakamani
Mi nisipo hangaika atayenilisha nani
Wananichekea usoni, kisogoni wananisema
Wanatafuta mabaya, wanjifanya hawaoni mema
Kisichoniua kitanikomoza ki-askari
Unavyo nichukia unadhihirisha mi mkali
Sina haja ya kurudia, Fiddy alishawaambia
"U-superstar mzigo wa mwiba" ukiubeba unaumia

(Langa langa, langa kilanga?)
(Kajinga tu kale) (..Ye mwenyewe mshamba tuu)
(eti, kabosi kale, ..yaani mimi kalanga kale..)
(Machizi wamemsaidia kishenzi.. wamembeba mpaka wamemchoka)
(..Sio inshu yule aah sio inshu yule..)
(..uhh, kichwa chenye utadhani madenge..)
(na na nanilii ngoja nikwambie, unajua eti enzi zile...)
[Hook: Langa]
Kila mtu Langa hivi, mara Langa vile
Yaani Langa tuu, yaani Langa tuu
Kila mtu Langa hivi, mara Langa vile
Yaani ni hayo tu, huh, ni hayo tu

[Outro: Fid Q]
Na nafuata njia zangu kama Carlito
Nayajua mateso kama Mel Gibson na Apocalypto
Na nafuata njia zangu kama Carlito
Nayajua mateso kama Mel Gibson na Apocalypto