Fid Q
Bendera Ya Chuma
V E R S E 1:
(Fid Q)
Naitwa FAREED.. Kwa maana mie ni wa kipekee na wa aina yake/
Huu UJASIRI na huu UTAJAIRI WA MASHAIRI una tafsiri zake/
JASIRI coz SIOGOPI kuumia/
Nikiwa na NOTI hutumia/
Akina KIDOTI wakiniaproach huwakazia/
TAJIRI WA MASHAIRI.. Mie sio hodari wa kurap tu/
Mie sio msanii, naifanya hii kwa ajili ya watu/
Nina USO WA MBUZI.. Na ninapewa front page/
Na DAILY kwenye NEWS sina skendo yoyote/
WAPI? WAPI? WAPI? WAPI niliwakosea?/
WAPI mie siku-play fea (fair)??
Sikuzaliwa niwe KAMILI nilizaliwa niwe REAL yeaah../
Na UDHAIFU hauna DILI ikiwa ni STRONG najiFEEL here/
NADHIFU KIAKILI, STREET SMART… BLACKSHAKESPEARE/
Nipo ili nife, MAISHA sio mchezo wa UWOGA, MJOMBA/
Unataka nishibe? Hakikisha haukombi MBOGA BOMBA/
Nipake TOPE..NIJIKOMBE, NIKUOMBE MAFUTA/
UNIPONDE..UNIZONGE KUTWA,NIKONDE MNYONGE WA KUTUPWA/
Kwa MGONGO WA CHUPA nipake nisije kupauka/
Nitaibuka tu kama vumbi.. DONGO likija kukauka/

H O O K
(Ben Pol)
Ninateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/
Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/
Nateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/
Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/
BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA
BENDERA YA CHUMA…
BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA
BENDERA YA CHUMA…
V E R S E 2:
(Fid Q)

Ninachunga HASIRA isiniumize ili MAUMIVU yasinitishe/
Hawaishi HILA wenye WIVU wananizingira nisipite/
DUA haziishii ANGANI/
UA linazaa BUSTANI/
BAHATI haina AHADI ikihitaji hutua NDANI/
SIHOFII kudondoka sababu mie nina MABAWA/
Waliofikiria nitachoka.. wanaogopa.. NGOSHA ana POWER/
CHEUSI ni mzawa.. CHEUSI ana DAWA ya kutoka/
Pagawa ukinitosa.. KOSA kunawa kabla haijatosha/
Kivipi UNIACHE wakati huu MZIKI uko na mie na kwake nina MAPENZI YA MSWAKI, Sitaki mwingine achangie?/
MASIKA bila MBU.. sio GHARIKA bila NUUH/
SHIDA anazo kila MTU.. CHAKARIKA uje UNAFUU/

B R I D G E
(Ben Pol )
HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/
Na pia ukishinda usijiboost.. usijiboost.. yanini makuzi/
HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/
HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/


H O O K
(Ben Pol)
Ninateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/
Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/
Nateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/
Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/
BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA
BENDERA YA CHUMA…
BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA
BENDERA YA CHUMA…
V E R S E 3:
(Fid Q)

Ninawafanya wanaKAA.. kama yule MC wa Kenya/
Ukisikia PAA.. ujue haikupangwa UFE mapema/
Sikuiti SHUJAA.. kwa kufanya kile unachofanya/
Nitakuita MJINGA.. ikiwa UKISHINDWA wakati CHAWEZEKANA/
DUNIA ni kubwa pia ni ndogo kama TUKIUNGANA/
KIUTUUZIMA.. Na MLIMA haupandwi, kwa KUUTAZAMA/
Ningekua KISIWA..MAISHA yangu yangekua ufukweni/
Huu upeo NIMETUNUKIWA na MUNGU wangu basi nipokeeni/
INATOSHA? Wanasema ‘ HAPANA ‘ DONDOSHA../
Na tena wanaochana.. hawajiiti CONSCIOUS ni NGOSHAZ