Rich Mavoko
Najuta
SONG:NAJUTA
ARTISTS:STAMINA FT RICH MAVOKO
PRODUCER:KEVY
STUDIO:SNAP RECORDS
SONG WRITER:STAMINA&RICH MAVOKO
INTRO
Stamina;iz moro town baby,im back,u know wat kevy,this iz so matured meeeen
Vers 1{stamina}
Shida zinaomba urafiki,umasikini unaleta posa
Ukubwa meli ya kigiriki,nimezamia bila boxer
Bikra ya utoto,imeshavunjwa na balehe
Ukubwa una mingi misoto,na mchanganyo wa starehe
Mara ooooh baba kijacho,eti niandae hela ya nepi
Wife anatoa macho,anangoja shopping ya sketi
Hakimu ana nyundo ya noti,mtuhumiwa nasaka chenchi
Bongo mahakama za joti,me mpoki nabaki benchi
Hata nikimchukia baniani,kiatu chake kina mchango
Mzinzi na nyota ya kijani,ndio uzazi usiokua na mpango
Balehe noma,kama baunsa aliyepigwa na mtoto
Ukubwa mechi ya kisodoma,haiwezi chezeshwa na mpoto
Aaaaah kas na kas,ni kasi isiyokua na kasi
Ila nikiweka kas na kus,ndio kusi pacha wa kasi
Bora wewe jalala,me ukubwa shimo la choo
Ukichanganya na ufukara,ndio mechi isiyokua na droo
Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe
Vers 2{stamina}
Maisha ngumi ya bitozi,siogopi kutega sura
Pesa sitafuti kwa pozi,bado najinyima kula
Nishachoka kusadiki,tomaso tangu na tangu
Marafiki wanafiki,wanasnitch hadi kwa mke wangu
Majukumu ya familia,nimeyabeba bila ngata
Asili zimezidi mia,desturi zimenikamata
Haya maumivu ya mjeledi,kwenye ngozi ya mlemavu
Ukubwa mechi ya mabaamedi,me mlevi nafungwa kavu
Aaaah maisha jabali,ugomvi wa cheka na Tyson
Sikuhizi ukinunua hata kagari,kitaani unaitwa free mason
Maumivu ya sufuria,jikoni hayana ushuru
Pesa tajiri wa dunia,mwenye hisa yangu ya uhuru
Aiseh sayansi imenikera,ukuaji umenipa msoto
Utu uzima bila hela,utamwamkia hadi mtoto
Napopata mkwanja,na shida zinagonga hodi
Vipi nitanunua kiwanja,huku bado nadaiwa kodi
Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe
Vers 3{stamina}
Ukubwa msafara wa kenge,me mjusi vipi unichoshe
Penzi kitovu cha uzembe,nakaza nisiitwe ngoswe
Ugangstar bila hela,majibu yake ni uchafu
Maisha ya bongo msosi wa jela,so mfungwa usiulizie ndafu
Nilizoea kashata,bumunda na vibagia
Huku unga,bangi,na bapa,ndio vitu navyovisikia
Chuki na fitina,hadhina za wenye wivu
Wapo wanaonishirikina,ili moto nigeuke jivu
Udogoni nilidekezwa,wazazi walinipa malezi
Pesa imesomea udereva,inaendesha hadi mapenzi
Elimu ya njia za panya,inanikosesha michongo
Madeni yananiandama,kama serikali ya bongo
Maishani ukiwa govinda,wenzako watakuita yaya
Pesa mnyama anayewindwa,na jangiri aliyevuta kaya
Uwazi unanidondosha,bado narushiwa kombora
Condom ndio kinga tosha,sijikingi na bastora
Choruss{rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe
Bridge{rich mavoko}
Heri ningerudi utoto,ujana maji ya moto
Eeeeeeeeh eeeeeh eeeeeeeh eeeeeeeehhh
Me najuta kubalehe,me najuta kubalehe eeeeeeh,me najuta kubaleeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhh
Ontro{stamina}
Moro in da house,in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Ahahaha I luv hip hop