One The Incredible
40 Barz
Habari mnoko/ Nina habari moko/
Huwezi timiza kazi kama askari choko/
Juu ya daftari ninatafakari msoto/
Kwa mistar mitamu kawa cadburry coco/
Hii ni classic, move kama dance/
Nawapa hisia kali zaid ya muvie za mikasi/
Kwenye chart zao wao washindani mi nafasi/
Sifanani nao mimi ni zao wao ni nyasi/
Mwanaharakati ka` kikosi na siasi/
Mistari ina siri nzito kama boksi la risasi/
Siko cocky nipo confident consciously active/
Kwenye booth niko lost kama park ya jurassic/
Geneous niliefeli ku-pass Mathematics/
Kama rap ni drug mi nna Habit kama addict/
Spit kama rabbit kwenye 8 mile
Love or hate it hardly debated hii ni anytime classic/
Verse balanced ka account ya fisadi/
Kwako mlevi wa u-star kama round za vinywaji/
Dunda kavu au bounce na kinywaji/
Skia biashara kwenye speaker naita sound za miradi/
Nna ujumbe mtam kama sound ya kingasti/
Snitch ask around niko down na illmatics/
Na-spit kwenye mic ka risas nipo kasi
So huwez pass around ka upo stuck kwenye traffic/
Aah... sibutui nashoot haswa/
Tui hujui siku zote vipi unisumbue kilaza/
Mdundo mweusi nausugua kama nna msasa
Mpaka duke ateme slang kama movie ya kihustler/
Hii kwa wote wanaoikubali sio flani na flan waipende/
Mi ndo moko makutano ya mistar kama stand ya mwenge/
Yafanya wengi waende mbali waache wachache wakae kizembe/
Kaa mbali nasi au kaa sawa nikulenge/
Sa kaa sawa snitch mi ni dawa ka G.V/
Hawa wanahisi ila hawapo sawa kama sisi/
Na kama mkavu hapa utanawa utakuwa mbichi/
Money ni power respect unaipata ukiijua na displine/
Kama kiongoz wa dini nampenda mjinga na mtoaji/
Kitaani wanga hunihofia kama bingwa wa uponyaji/
Linda chako mjinga watu wanawinda hawako safi/
Ukizingua unagongwa tako kama mznga wa konyagi/
Nampenda haswa anahisi anaijua heshma/
Daktar rudia darasa mimi ni ugonjwa usio na jina/
Anashangaa dina mara hawa mara huyu we ni buyu mi ni moko sawa sawa...