One The Incredible
Haya Maisha
Intro;
Yo, M-Lab, One
Uh, Mujwahuki, Den Tex
Yo, Cheki

[Verse I: One The Incredible]
Bado njaa uswahilini
Napo kaa panatisha, mpaka nashangaa kuwa mimi
Hapa hapa mjini bado kuna nyumba za udongo
Mama hana mchongo mpaka ana amua auze gongo
Ili dogo aende shule
Nakule hakuna walimu, ina gharimu hela ndogo iende bure
Utachanganyikiwa na maisha
Hivi lini nami nitafanikiwa kuwa fisadi
Watoto wasome bure, shule nzuri
Huku dogodogo poa na mama watoto mzuri
Vimada kila mtaa kisa hela
Msela akishangaa sana mzigo, papaa namtupa jela
Kula sana mali, ishi kifahari
Ndani ya nyumba kubwa zaidi ya ofisi ya serikali
Huku kwa maskini hali ni kheri
Habari ya kweli, hatuna amani ya kweli
Ibada zinashawishi masikini wajifilisi
Ili kuwa tajirisha waajiri wa ibilisi
Uswahilini ukichunguza, bado njaa
Ni balaa, huyu Mungu wa Kakobe hana uchungu na mitaa

[Hook: Songa]
(Kamakawa si uchuni, bado zama ni duni
Wahuni hawana maana washazama na uchumi
Sijui nitafika au nitafichwa uvunguni
Ama nitaishia njiani kama picha ya kubuni) x2

[Verse II: One The Incredible]
Maarifa na mawaidha, faida ya afisa
Nyadhifa ikishika, ni maafa ya taifa
Pametanda giza, shida nchi imeota miiba
Wananchi wananyata kimaisha
Labda nitafika kwa imani
Ila inatisha, siku hizi siasa imefika ibadani
Nadhani zimeshafika nyakati
Muda umewadia, hii dunia imeshafika tamati
Sikia ujumbe, uwe mwenye nia safi
Ulie kufikia, hakukufikia kwa bahati
Utubu na ukumbuke
Kwamba maisha magumu, inakubidi uwe sugu na usumbuke
Uwakumbuke hata ndugu, usiwe bubu
Wavute karibu, haitogharimu, usiwatupe
Muumba nikumbushe, nikumbuke nielewe
Nijapokuta jaribu, wa kumkumbuka ni wewe
Nisamehewe napojuta kweli
Ni wewe nakutukuza, naposumbuka kuitafuta kheri
Ki ukweli yamenifika kwenye shingo
Kilio cha mzawa kimesikika kwenye wimbo

[Hook: Songa]
(Kamakawa si uchuni, bado zama ni duni
Wahuni hawana maana washazama na uchumi
Sijui nitafika au nitafichwa uvunguni
Ama nitaishia njiani kama picha ya kubuni) x4