Young Killer Msodoki
Run DSM
Beti 1:
Kwa jinsi navyoizinga rap, hawapiti majamaa/
Wanashangaa kuona kila biti natambaa/
Wanajiuliza yuko vipi huyu kachaa?/
Asante kwa mwenyezi maana niko fiti mpaka raha/
Wote ma mc viburi watakoma/
Kama rap ganja badi mpaka puli nishachoma/
Cheki time hii niko na Dully kwenye ngoma/
Machizi wanapiga yowe "MWANA NZURI MPAKA NOMAA"/
Mi ni mwendawazimu sifai katu/
Padri toka kuzimu nanywesha divai wafu/
Unayejifanya we ndo bingwa wa rap/
Haya potea, m-baya nishatinga kwa map/
Usifanye usiku nije "knock your doors"/
Naked with ma di**k straight like pinocio nose/
Coz, nataka nije run dsm/
And i dont' want to be the same/
So lets gooo.....

Kiitikio (Dully Sykes)
Eyo whatsap, haters na machizi wangu wote kwenye rap/
Mimi ndo mwenyewe na nshatimba kwenye map/
Ona nazitafuta nazo zaja chap chap...... Nataka run dsm
Na.... nana nanana nana naa
Nana nanana nana naa x 2

Beti 2: (Young Killer)
Mapenzi hayana shule binadam hatufundishwi kupendana/
Sijahit bure muda ule haikuwa rahisi kusimama/
Haikuwa njama nlikazana kibishi/
Sio kama rap ya kweli hakuna, ila wanaochana hawaridhishi/
Leo nakamua kikauzu/
Na najua kuwa hata akili inahitaji nguvu/
Ili i-move, nisonge mbele niwaache mazuzu/
Nawachenga ambao mtihani wa kubebwa wamefuzu/
Vinakera vikwazo, kipaji ndo chanzo/
Mziki hauna hela nlizotarajia kuwa nazo/
Futa mawazo, presha na aibu/
Sasa utapataje pesa, kama ukiwaza tu haupati jibu/
Nini maana ya muziki kama uwezo hautumiki/
Ukichana kupita kiasi unapoteza mashabiki/
Skia, nataka nije run dsm/
And i dont want to be the same/

Beti 3:
Unaweza kuwa na nyimbo tele, yah ukafanya nyingi/
Ila zote kelele zaidi ya kengele ya Misanya Bingi/
Mi nitadumu hadi milele kwa misingi/
Hadi siku navishwa suti tai mbele kama dingi/
Ukiniita "booth" haina kwere man/
Waulize wanaonijua kwenye rap niko very fine/
Tena huaga sioni gere man/
Sumu ya marapa mimi ya mapenzi muulizeni Belle 9/
Navyowapa shurba hawaamini/
Nawaganda kisawasawa zaidi ya ruba mwilini/
Mi ndio "Carbon", nikitimuka hawavuti hewa/
Levo zao chini sana ka bei za uchi sewa/
Wanasema nna sura ya kipedeshee/
Acha wale ujana maana mi ntakula mpaka uzee/
Skia, nataka nije run dsm/
And i dont' want to be the same/
So lets gooo