Young Killer Msodoki
Dear Gambe
Intro:
Na na na, na na na
( Mona )
Oh yeah, I don't know
I don't know, no
(MONA GANGSTER)

Dear gambe 'umefanya maisha yangu yayumbe
Mi ni mpambe wako leo nimekutumia ujumbe ( I don't know )
Mi ndugu yako nipe ukweli usinifumbe 'uwepo wako, ukaribu
Vipi unafanya niyumbe?
Kila muda kwenye friji unajiponza, mi domo zege nikishakutumia natongoza
Nalewa 'usiku kucha jua linachomoza
Nasindikiza na supu asubuhi njema unaniongoza
Wewe ni nani unaye iendesha hii akili?
Nikiwa na mawazo unanitoa stress nisifikiri
Ukiwa mezani chupa kadhaa sijiwezi mpaka mtaani washanipa jina jingine la mlevi ( Eh )
Unafanya na fubaa mi mwenzako 'hadi kazini naiba chapaa nije kwako
Dear gambe 'mitaa haipi ukweli wako, na kila ugomvi wa bar kwanini chanzo ni chako?

I wanna know 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey
I wanna know ( I wanna know, know, know, know, know ) 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey

Yeah, uh
Unafanya ndoa nyingi zinavunjika
Hasi chanya 'we na msosi nikichanganya natapika
Haukatai kila mteja anayе kualika
Unafurahi na ubaridi wa maji unachirizika
Likitokea tatizo 'wewe ndio kimbilio
Nnapo tinga nakuwa muongеaji bila mpangilio
Nasahau kinga tamaa ndio kimbilio 'we ni funda la ziada, unaniumbua mi mwenzio
Una nilainisha koo, ki fikra una nibembeleza
Una ni-control 'sijasoma naongea hadi kingereza ( I don't know )
Ushaniweza 'nani aliye kutengeneza?
Na nini aliwaza (?) ni mbaya kwa wasio jiweza
(?) nilikunywa kwa furaha, najikojolea unaniathiri na nnatoa chapaa
Dear gambe 'mitaa haipi ukweli wako, na kila ugomvi wa bar kwanini chanzo ni chako?
I wanna know 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey
I wanna know ( I wanna know, know, know, know, know ) 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey

Dear gambe 'una nichanganya sana
Una majina mengi mpaka ya mbuga za wanyama
Nashangaa 'mengine yanatia kinyaa, mfano mzuri; ni gongo, champumu hata chang'aa ah ( Hey )
Kwenye ubongo umetawala kila sekta
Ni ukweli; siwezi kuwa nawe bila pesa
Watu wengine wanakula ada kisa wewe ( Yeah )
Unawafanya wanasahau ibada ( Oh woah )
Na juzi juzi tu nimepata habari ( Oooh woaah... )
Kuna mwana ulikuwa nae ameshapata ajali
Dear gambe 'ni kweli unanichosha
Napenda kuwa nawe ila nyumbani mboga wanakosa
Nawaza jinsi gani nitakuacha, mpaka wazalendo wa dini baadhi kwako wamedata
Hakuna utata, poa 'sasa najikata kapuku nikizipata nitakufata

I wanna know 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey
I wanna know ( I wanna know, know, know, know, know ) 'umenipa nini
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey

I wanna know ( I wanna know ) umenipa nini
I wanna know
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey ( I don't know )
I wanna know ( I wanna know ) umenipa nini ( I don't know, yeah )
I don't know ( I don't know ) sikuachi kwanini, hey
Outro:
Classic sound, yeah yeah yeah yeah yeah yea yeah