Ken Ring
Mama
[Intro: Vigeti]
Aaaaaaaah!
Haa (sigh)

[Verse 1: Vigeti]
Hii ni barua yako mama
Mda mrefu tangu sisi hatuja onana
Niki kufikiria machozi huwa yana ni bana
Hope hivi karibuni si tutagongana
Walai hata mi sijui nitakupea nini
We ni zaidi ya mwanaume kunilea mimi
Shida zote nimepitia umeniwekea msingi
Na vile ma-………kubebea mpini
Ume-determine yule mwanaume niko saa hii
Alhamdulillahi asubuhi iko chai
Nashukuru Mungu kwa kunipa mtu kama wewe
Ulini guard ka vifaranga kumejaa mwewe
Afadhali tukule ndio ulale njaa
Wakati buda ana-kunywa-tu ma-barley bar
Though maisha haya mtu huenda akapagawa
Usijali mama mtoto wako ako sawa

[Chorus: Alicios]
Mama!
Hakuna kama wewe
Na yote uliyo tenda
Mama!
Nakukumbuka wewe
Mwanao nakupenda
[Verse 2: Vigeti]
Mtoto wako amekuwa
Tushukuru Mungu juu hapo hungenjua
Wanataka-tu kunipeana
Baada ya giza tu siku mpia imeaanza
Wanaeneza uvumi kunihusu
Mi ma-Judas Iscariot, wanataka kunibusu zi
Usiseme eti mimi nimepotea
Hii star yetu shindwa ni lini nitatokea
Ushanitafuta sana nime-lostia madawa
Ni na vuta prama
Ma! Maisha ishaenda haywire
Siku hizi mi naonanga kila day mbaya
Najaributu ku-maintain
Kuna maswala ndoto ndio ni stay sane
Serekali kwa case yangu wana-ni-geh chase
Nashindwa form ni gani!

[Chorus: Alicios]
Mama!
Hakuna kama wewe
Na yote uliyo tenda
Mama!
Nakukumbuka wewe
Mwanao nakupenda

[Verse 3: Vigeti]
Mama, siku hizi wamekuwa wanyama
Kila saa sio wale tulikuwa tunajua jana
By the way na ku-miss tu
Shish anakutumia ma-kiss through
Anashindwa atakuona lini
Ashakuwa mkubwa ana soma msingi eh!
Ana-miss nyanya yake
Hata kama mamake ali-diss baba yake mmh
Mambo si sawa ile kitu inaharibu mtoto wako ni dawa
Kusema ukweli mi na-regret
Juu najua saa hii nafaa ku-live great
Ni wengi hatuko nao
R-I-P watu wako kwao
Naomba Allah anisamehe
Aniepushe na ni-msalah kila tarehe


[Chorus: Alicios]
Mama!
Hakuna kama wewe
Na yote uliyo tenda
Mama!
Nakukumbuka wewe
Mwanao nakupenda
Mama mama mama mama maaa!
Hakuna kama wewe
Tutaonana tena