A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #

Fid Q

"Mzee Mbuzi"

Mzee Mbuzi wewee!

[Verse 1]
Hii game ni yako, Hizo ndiyo kauli za mitaani/
Haufiki sehemu bila ku-Hustle, Hivyo walinishauri nipambane/
Nauli nisakanye, Maisha ni safari nijihami/
Ball so hard maths, Kuwa na fani/
Yes, kipindi ya mchonga niliishi fresh kabla ya ruksa/
Mshua hakuwa na stress, Alilaza cash usiku kucha/
Ghafla akawa haonekani nyumbani, Shida zikatupa fursa/
Ikawa msafi ana zamani, Basi mchafu naye ana future/
I remember, Enzi zile uso wa mbuzi ndiyo unapendwa/
Silipi nauli kwa mikwara, Na uki-move nakutenda/
Kwenye daladala, Konda fala asije nitenda/
Mi ni staff ka nyapara, Huko bara nisha-surrender/
Nilichotaka nifike studio/
Ni-record muweze nipata kama busta au kuriyoo/
Sikuwa na pozi za kirapa nilikuwa Gangsta sijui Yooo/
Nikawa conscious, Mtu wa culture, Rasta ambaye haangui ng'oo/
{Cough}
Niliyoanza nao ni kama hawataki huu mchezo/
Eti unahitaji zaidi ya bahati, Yaani kismati na uwezo/
Haufuati vigezo/
Unapoamua huchuja hadi wanaojua/
Natukuzwa nawazingua, Ukiuchunguza utagundua/

[Chorus]
Mzee mbuzi weee... Wee! Wee!
Wewe... Wewe... Wewe... Wewee
Mzee mbuzi weewe..
Wewe... Wewe... Wewe... Wewee
Ni wazi haikuwa rahisi, But you made it
Mzee mbuzi wewee...
Wewe... Wewe... Wewe.. Wewee

[Verse 2]
Ukishajua nini unataka, Nini chahitajika ili ukipate/
Kamilisha mahitaji kisha kifuate/
Sikuwa humble mbele ya wajeda pale mnafiki akizingua/
Kivuli cha unyasi, Hakimzuii mtu jua/
Mi na-hustle ile ki heavy weight/
Skendo haziwezi mnyea Fid/
So fragile and delicate, Handle with care.. Care/
Bado sijafeli eti, Mjengo unaniteta street/
Kama Makaveli nikifanya kweli zinaenea hit/
Kinachowaponza watoto wa mjini ni tamaa na mikumbo/
Macho huonja kabla ya ulimi, Na wana njaa zaidi ya tumbo/
Kataa kuwa kaa, Kataa kukaa kaa/
Bila chapaa, Kitaa hautong'aa papa/
Ninavyotembea ni kama hero wa kuitwa Che Guevara/
Navyozisaka hata nikipata, Zero inakuwa sio ya duara/
Hai-make sense kama haileti dollar/
Mwache waiter a-keep change, kama waitress fala/
Yote haya yalikua ni utoto juu ujana/
Yalianza na maamuzi ya utoto kuukana/
Yakafuata makamuzi ikawa moto juu sana/
Tukawaacha wenye makuzi bila soo huku wakitukana/
Wana hate coz siwezi afford kufanya mistake/
Wanacho otea hawa matozi, Of course, Kinaonekana kime shake/
Muda niliusoma kwa jua kabla ya Jaco kuyajua/
Saa hii kila ngoma wanaipakua, Inaipa macho Medulla/

[Chorus]
Mzee mbuzi weee... Wee! Wee!
Wewe... Wewe... Wewe... Wewee
Mzee mbuzi weewe..
Wewe... Wewe... Wewe... Wewee
Ni wazi haikuwa rahisi, But you made it
Mzee mbuzi wewee...
Wewe... Wewe... Wewe.. Wewee

A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #


All lyrics are property and copyright of their owners. All lyrics provided for educational purposes and personal use only.
Copyright © 2017-2019 Lyrics.lol