Fid Q
13
VERSE 1:

Mama ndie alie nitabiri mi nitakua star na nyota wa kila pande/
Nikiwa na raha.. kwa mwenye hasira nisijigambe/

Usimpige mkeo piga shangwe/

Kwa maana Young killer sio ngazi.. kwa hiyo mwambieni shetani asinipande/

I Think big.. its my dream biggie kuwa/

Bigger wa michano n***a ambaye hata Jigga atanijua/

Kuwa msodoki nawaficha mistari/Upeo wangu umekula mchicha na ndo maana nina fikra za kuona mbali/

Msukuma anae sukuma mitikasi ikatulia/

Hata ' Francis Cheka ' naweza mpiga panchi akalia/

Wanaoijua njaa ndo wanaamini cha kwanza kilimo/

Mi sijagombania ustar ili nikifa nikazikwe kino/

Wabovu wakichana ' IMO ' na hawazijui nguzo tano/

Leo kwenye ustar ' simo ' kisa sina muonekano?/
Mi nina POWER.. ya ibada nilioiomba baada ya kipato/

Pole dada ulie nitosa kisa umenizidi kidato/

Futa jasho na damu saka noti 'hali tete' /

Watoto wanamjua Diamond na Joti"" zaidi ya Kikwete/

Popote niko fiti...tega skio/

Shoga hata akitoa jicho vipi...hawezi kuyaona mafanikio..ndio


Chorus:

Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/
Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/
Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/
Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve





VERSE 2:
Wakisha amini unawahitaji zaidi ya wanavyokuhitaji/
Mapenzi ya ' wadau wa mjini ' hugeuka ya ' samaki na maji '/
Uishi ndani yake tu... nje yake uvuliwe/
Kwa msaada wake upikwe kisha yawanawishe.. uliwe/

SIKUUMBWA nije kusettle for less/
Nitaisubiri mvua inyeshe.. nijitokeze kudance/
Nonsense sitemi/ asset sio deni/ HOMEBOY.. natema vitu on point.. jifunzeni/
THAMINI HUU MUDA kabla haujageuka HISTORY/
Part of the PAST dont fit the script for the FUTURE memory/
Niliyoyapitia... yameniandaa kwa haya yajayo/
Sio dalili ya kusinzia.. ni ' NJAA ' nikipiga mihayo/
Sina JEURI wala MZAHA wa kugeza tabia mbovu/ Nina KIBURI cha JERAHA ukinipoteza ninaacha kovu/
MASKINI.. ninajiamini hadi natokwa na ukungu/
Bila ujuzi wasingenithamini.. NINGETOSWA mpaka na ndugu/
Kitachonizamisha sio kudondoka mtoni/
Ni kushindwa kupiga mbizi na kusizi ili msinione...



Ni MSODOKI na NGOSHA.. Miujiza iliyotabiriwa haina haja ya kuogopa/
Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi/Lakini ninaweza zitengeneza nikiongeza juhudi/
Tangu Agosti tangu April.. YEAAAH.. tangu Agosti tangu April/
Nina Hustle bila wasi wala hofu/ MUNGU wangu hawezi nipa shida ambayo nitashindwa kuisolve

VERSE 3:

FQ-
Napenda umaarufu.. ninachukia MBWEMBWE zake/
Au ninapospit truth kwa booth halafu WAKUSHI hamninyaki/
Ninauacha uchi ' UKWELI ' uzushi sio mwake/
Hata mkigushi mtafeli.. hamnigusi na hamnipati/

YK-
Siamini nimekua MIMI hadi hii leo nimefika hapa/
Aliyenilea hakuniamini.. niliyemtegemea hakunitaka/
Bila nyinyi.. WADAU.. Ninakili sishiki sarafu/
Na ndo maana sili bata kwa maana BATA WACHAFU/
Kuwa mkali wa kusifiwa.. kubali kutumiwa/
Nilichoambiwa kuwa ' sikuhizi hadi wajanja wanaliwa'/
Inatakiwa kuwa STRIKER..Mambo yaende SCHKOPA/
Kama haujanileta.. hauwezi kunirudisha nilikotoka...