WACHUJA NAFAKA Featuring FID Q - "Ukweli Na Uwazi" lyrics
[Instrumental:]
[Verse 1: Juma Nature]
Hisia zangu zinagota kwenye stimu za kulanduka (nduka)
Halafu msumbufu bwege eti unataka kuni-change mzuka (mzuka)
Khalfani prodyuza' P Majani
Naomba uniongezee jani
Halafu mwambie (?), boya ani (?) ubani
Utadata...Si dati
Utadata...Si dati
Aya bwana lakini kumbuka picha linaendelea
Usije kuharibu nyimbo' hili ni Apple la kijani
Punguza mori, Majani
Tuisawazishe hii hali
Tusali kabla ya hasara' tukichelewa tutapigwa mawe (mawe)
Na ndo mtindo ambao uta wafanya walokole tupagawe
Midaa isha kwenda na hakuna atakaye mlinda mwanae
Kama unaringa; Haya we...Haya we...Haya we...Haaa...
Ukija kwenye suala la mlo' utakuta ni kasheshe
Ukitaka kujipatia ridhiki' lazima ukeshe (lazima ukeshe)
Unyonyeshe' Ayaah...
Hali si hali' dunia imegeuka kaa mbali
Wanafunzi mtumwe,msitumwe' hatusomi bila shing' kumi
Mwalimu badala ya kufundisha; Moja...Mbili
...Tatu...anatufundisha uhuni
Si ma...si maji ya ukoko hayo?
Wananchi wotе mateso' japokuwa raha kidogo wanapata
Ifikapo tenda nadata
Mbishi naamka asubuhi,sijanawa uso,chai sijaona,sijapiga mswaki
Tokea mdaa ulе ambao nilikuwa shule ya msingi
Na biashara yangu kubwa ilikuwa ni kuuza karanga; na Ganja
"Yote ni sababu ya njaa yetu na shida na matatizo ya dunia"...
[Chorus:Juma Nature]
Huu ni ukweli na uwazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
Huu ni ukweli na uwaazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
[Verse 2: FID Q]
Siku hizi uwizi' hupewi mkong'oto
Ni unyama uliokithiri, sio siri' huchomwa moto (Unongwa huo,Unongwa huo)
Wanavuliwa nguo' kisha wanaonjeshwa joto
Wakati Bongo life msoto' umeona? Na umeshajua
Anapopigwa na wananchi, hamna sheria' hamna hatua
Mikononi akawafia
Wallahi' namna hiyo haifai
(Wallahi' namna hiyo haifai)
Kwanini msimkate mkono na kumwacha akiwa hai
Au labda apewe msaada
Anayemjua' asimshangae, umeona eeh
Majani vipi nachoma eeh (eeh)
Hii habari nzito
Wanakiuka miiko,wakati ni ukweli na uwazi
Hali sio hali' ndani ya kumi bora za mjini' maskani wana njaa kali
Hamjajua mtakula nini, halafu nyie mnaponda mali
Hivi hiyo ni nini?(nini)
Utajiri nguzo ubahili' hivyo ndivyo mnavyo amini
Mmesahau kiama ni lini, au mmesahau mafunzo ya kidini
Yaani matunzo kwa vipofu, vilema,mabubu,viziwi
Maskini ambao' wapo vagaranti, bankrupt' hamu wathamini
Nyie ni uzinzi na uasherati
Hivi kesho mavumbini' tupigwe chini wenye vidogo, vidogo serikalini
Hivi mme (?) kuwa ondoa ma kaka poa wa hapa mjini
Kama mlivyochokonoa na kuwa komoa watoto wa mjini
Kwa kesi ya uzururaji na mashtaki ya kubuni
Ukweli Na Uwazi' hizi habari sio uvumi (sio uvumi)
Imechafuka bahari, damu ya mvuvi na nyangumi
Alipo mhuni' akija askari ni ngumi
Hali sio hali' hizi nyingine basi kapuni...
Whoa...
[Chorus:Juma Nature]
Huu ni ukweli na uwazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
Huu ni ukweli na uwaazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
[Verse 3: Juma Nature]
Mpogo Juma Mpogo' naomba nimuulizie Zogo
Jamaa kanidunda sana mpaka kaniumiza chogo
Mkono umevunjika tena' wakati jana nimetoa muhogo
Na kumbe watu wana kufa hivi >> hivi
Nitoeni hii roba' mwenzenu mie nakata roho
(Fixing up his throat)
Naona sasa afadhali' nishaitoa kabali
Japokuwa nimeumia lakini bado nachimba biti
Wewe mtoto bahati yako sana nimeteleza na kiti
Na tusikutane (?)
Ombea shetani wangu apite (shetani wangu apite)
Kumbe mzee hapa nunda "nimeshukuru kweri"
Zilibaki sekunde chache tu nilikuwa nakufa kweli
Huu ulikuwa muda ambao bado shule ya msingi
Maisha yalikuwa mabaya' dingi hakunipa hata shilingi
No sweat! Hamna noma, sasa naona (?) unapoona
Kivumbi kwa maskini wasiojiweza na wana dini
Wana angamia kirahisi' kama sio visa ni nini?
Waekee basi genge la samaki kibua' kwa ubwabwa
Haya basi, wasaidieni vipande vya sabuni' hamtaki
Haya basi, wakodishieni trekta wakalime...
[Chorus:Juma Nature]
Huu ni ukweli na uwaazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
Huu ni ukweli na uwaazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
[Instrumental:]
[Chorus Repeat:Juma Nature]
Huu ni ukweli na uwazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
Huu ni ukweli na uwaazi...
Huu ni ukweli na uwazi...
Wananchi tunashindwa vumilia' ila tu tunabaki tunalia...
[Instrumental]