VERSE 1
Alizaliwa mashariki alifahamika mahali pote
Alikuwa malaika wa ndoto zetu wote
Walimwita Mwanajua kwa maana alijua vyote
Alitamalaki nuru ilitua mahali kote
Na kila mahala alipita watu walimuheshimu
Hakwenda shule ila aliheshimika ka’ mwalimu
Alikuwa mzuri kweli lakini shobo hana
Hakuna aliyemgusa kwani alikuwa wa moto sana
Urembo ulimuweka juu hakushuka anga zetu
Alikuwa maarufu kushinda hata bwana Yesu
Hata watoto walimpenda walifanya sherehe
Tuliobalehe alipopita tulimwaga mbegu
Ilipofika asubuhi tulimuwaza yeye kwanza
Ilikuwa ni kama desturi kumfata
Tulikuwa hatuli tukasaza
Tuliwaonea wivu rafiki zake Mekuli na Veneranda
Walikuja madogo wajanja na mapesa
Wakauliza mama ukivaaje unapendeza
Wakamuahidi ndizi, mawaridi na hariri
Lakini jasiri rangi yake ya asili ilitesa
Warembo wa dunia na vivazi vyao
Waliwaza kumfikia na ilibaki njozi kwao
Wazungu walikuja na pozi kibao
Walimkaribia mwisho walibabuka Ngozi zao
CHORUS
Mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
Mwanajua..ameondoka kama hakuja
Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo
Kitakuwepo tu kwa muda
Mwanajua…Mwanajua…Mwanajua…
VERSE 2
Tulijaribu kutumia chambo
Apite anase ili tuweze kutupia mambo
Mitego iliwekwa aje atumbukie hapo
Tuliishia kumwona mbali na mwisho kuumia macho
Haki ya nani, kuna walo’diri kumwita Mungu
Walitukuza walisadiki na kuabudu
Na sisi alitupa nguvu
Tuweze kupambana kutafuta pesa ili tu tuweze kummudu
Manyoka waliyavua magamba yao
Wapendeze ili waje waweze kupata fao
Walitanguliza vyeti na madaraka yao
Waliisha kufa tukawazika na haraka zao
Licha ya utofauti wake
Alikuwa mkimya hakuna aliyeisikia sauti yake
Wenye wivu walichoshwa na mizingu
Maana alingáa sana kiasi alizificha nyota kama wingu
Naziwaza features zote complete
Nilitazama sikuona diva wa ku-compete
Bila ina ala make-up za kisasa
Aliwaka sana.. mtoto Fulani konki
CHORUS
Mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
Mwanajua..ameondoka kama hakuja
Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo
Kitakuwepo tu kwa muda
Mwanajua…Mwanajua…Mwanajua…
VERSE 3
Yeah!
Iwapi barabara isiyo na kona?
Simulizi isiyo na mwisho?
Makala zimeandikwa tupo na nakala tunasoma
Imeandikwa upasuka inapovuma sana ngoma
Vile alikuwa amesukwa ni kwere
Alipofika ilikuwa ka’ umeshushwa umeme
Kwa uzuri utadhani amejiumba mwenyewe
Tulihisi hatashuka milele
Tulikosea kwani…zile sifa hazivai tena
Imefika jioni na yeye hang’ai tena
Ndege hawaimbi nyimbo, misa zimefungwa
Wamwaga mbegu wote tumebaki dilemma
Najiuliza, alifichwa na ndugu kwenye kaya?
Au alinenepa kutoka aliona haya?
Hakujua, tulishindwa kutafakari chanzo
Maana alizima na hakuwa wa moto kama mwanzo
Anatukumbushwa kuwa tayari inapofika zama
Hatamu yake imefika, zamu yake imekwisha
Hajaacha hata alama ya damu yake
Amekufa na utamu wake Yarabi nasikitika sana
Namkumbuka sababu hakudanganyika
Nuru yake pahala pote ilitawanyika
Toka mzizima pwani kote alipagawisha
Aliondoka na mwisho alionekana ziwa Tanganyika
Dhahania zimeandikwa alichoka pengine
Aliondoka ili wang’ae nyota wengine
Itakufa damu, itakufa nyama
Nenda mwanajua nenda tutakumbuka sana
CHORUS
Mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
Mwanajua..ameondoka kama hakuja
Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo
Kitakuwepo tu kwa muda
Mwanajua…Mwanajua…Mwanajua…